-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

STRAIKA wa kimataifa wa DR Congo, Kadima Kabangu ambaye anakipiga katika kikosi cha DC Motema Pembe ya nchini humo, amefungukia dili lake la kujiunga na Yanga.

 

Kabangu ambaye amekuwa kwenye rada za Yanga kwa muda mrefu, amesema hawezi tena kutua kwenye kikosi hicho kutokana na masuala ya fedha.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kabangu alisema yeye pamoja na viongozi wa Yanga walishindwa kukubaliana katika masuala ya fedha huku akidai fedha ambazo alizihitaji viongozi waliona ni nyingi jambo ambalo lilipelekea dili hilo kuishia njiani.

 

“Tulikuwa tupo katika mazungumzo mazuri na Yanga katika kukamilisha usajili wangu wa kujiunga nao, kwangu mimi sikuwa na shida na tayari nilikubali kuwasikiliza ili kama mambo yangefanikiwa basi ningejiunga nao.

 

“Kilichokwamisha mimi kukamilisha usajili wa kujiunga na Yanga ni masuala ya fedha, ofa ya Yanga ilikuwa ni ndogo kwangu na ofa ambayo niliwapa mimi nahisi waliiona kubwa sana, mwisho wa siku nikaona wapo kimya nadhani hapo ndio mwanzo wa dili kuishia njiani na kushindwa kukamilika,” alisema Kabangu.

The post Straika Mkongo Afungukia Usajili Wake Yanga SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand