-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, John Bocco na mlinzi Ibrahim Ame wanatarajia kuukosa mchezo wa leo wa kundi D, kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), kati ya Stars na timu ya taifa ya Guinea utakaopigwa leo nchini Cameroon.

 

Mchezo huo ndiyo utakaoamua ni timu gani baina ya hizo ambayo itafuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo Stars inahitaji matokeo ya ushindi ili kufuzu.

Wapinzani wa Stars, Guinea ndiyo vinara ambapo wamejikusanyia pointi nne sawa na Zambia wanaokamatia nafasi ya pili wakipishana kwa tofauti ya mabao huku Stars wao wakiwa wanakamatia nafasi ya tatu na pointi zao tatu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa kikosi cha Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema: “Ukiachana na Erasto Nyoni ambaye amerejeshwa nyumbani Tanzania kwa matibabu zaidi.“Tunatarajia kuendelea kukosa huduma ya wachezaji wetu wawili ambao ni nahodha John Bocco na Ibrahjim Ame katika mchezo wetu wa kesho (leo) dhidi ya Guinea.“

Wachezaji hao bado wako chini ya uangalizi wa daktari kutokana na majeraha yanayowasumbua lakini yapo matumaini ya kuwatumia kama tutapata nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali,” alisema Cannavaro.

The post Stars ni Kufa Au kupona Cameroon Leo appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand