KLABU ya Simba imemsajili beki kisiki Peter Muduhwa aliyekuwa akikipiga katika Klabu ya Highlanders ya nchini Zimbabwe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Simba imeandika; Karibu kwenye familia kubwa ya mabingwa wa nchi beki kisiki Peter Muduhwa (Master of Defense). Wanasimba tunakupokea kwa mikono miwili na tunaamini utatufanyia kazi kubwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Simba Super Cup.
Muduhwa ambaye alikuwa anachezea Highlanders F.C ya Zimbabwe amejiunga na kikosi chetu akitokea Cameroon kwenye kikosi cha Zimbabwe ambacho kinashiriki CHAN.
The post Simba Sc Yashusha Jembe Tena appeared first on Global Publishers.