Simba ni Raha Tupu, Yawapiga Wazimbabwe -(Picha + Video)-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba ni Raha Tupu, Yawapiga Wazimbabwe -(Picha + Video)-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

SIMBA ni raha tupu huku Kampeni ya WIDA ikijibu Uwanja wa Mkapa jijini Dar jana Jumanato baada ya Simba kupindua meza mbele ya FC Platinum kwa ushindi wa mabao 4-0 ambayo yameifanya isonge mbele hatua ya makundi ya mi-chuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mbinu za Kocha Sven Vandenbroeck ambaye alianza na mshambuliaji mmoja, Chris Mugalu, zilijibu dakika ya 39 baada ya viungo Luis Miquissone na Clatous Chama kupeleka mashambulizi yaliyofanya Luis achezewe faulo ndani ya 18.

 

Mkongwe Erasto Nyoni hakuwa na huruma baada ya kumtungua kipa wa FC Platinum kwa penalti ya viwango na kuifanya Simba iende mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao 1-0.

 

Bao hilo likaweka mzani sawa baada ya mechi ya kwanza kule Zimbabwe, FC Platinum kushinda 1-0.Kipindi cha pili FC Platinum walifunguka na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, pongezi kwa kipa Aishi Manula ambaye aliweza kuokoa michomo ya hatari iliyokuwa inatengenezwa na muuaji wao kwenye mchezo wa kwanza kule Zimbabwe, Perfect Chikwende.

 

Beki mkongwe, Shomari Kapombe aliandika bao la pili kwa mkwaju matata baada ya kipa kutema shuti la moto lililopigwa na kiungo Larry Bwalya nje ya 18, dakika ya 62.

Dakika ya 90+1, John Bocco ambaye aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Meddie Kagere ambaye aliumia muda mfupi baada ya kuingia akichukua nafasi ya Mugalu, alipachika bao la tatu kwa pasi ya Bwalya.Chama alimaliza msumari wa mwisho dakika ya 90+5 kwa penalti ambayo alifanyiwa madhambi yeye mwenyewe ndani ya 18. Simba ikajihakikishia ushindi wa mabao 4-0 na kusonga mbele kwa mabao 4-1.

Luis na Chama walikuwa nyota huku Said Ndemla ambaye alichukua mikoba ya Jonas mkude mambo yalikuwa mazito kwake kwa kuwa hakumaliza dakika 90.Ushindi huo unaifanya Simba kucheza mechi tisa nyumbani katika michuano hiyo bila ya kupoteza. Matokeo ya mechi hizo ni; Simba 4-0 Mbabane, Simba 3-1 Nkana, Simba 3-0 JS Soura, Simba 1-0 Al Ahly, Simba 2-1 AS Vita, Simba 0-0 TP Mazembe, Simba 1-1 UD Songo, Simba 0-0 Platea United na Simba 4-0 FC Platinum.

Simba kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo, ina uhakika wa kuomba kitita cha dola 550,000 ambazo ni sawa na Sh Bil 1.2 za Kitanzania ambapo Shirikisho la Soka Afrika (CAF), huzitoa kwa timu zote zinazotinga hatua hiyo kwa msimu huu.

The post Simba ni Raha Tupu, Yawapiga Wazimbabwe -(Picha + Video) appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.