-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BEKI wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amesema anashangaa kuona mashabiki wa timu hiyo hawaamini, lakini ukweli ni kwamba sasa wanawania ubingwa.United walikaa kileleni kwa mara ya kwanza juzi baada ya kufanikiwa kuwachapa Burnley bao 1-0 na kufikisha pointi 36, tatu mbele ya Liverpool.

 

Neville amesema ameona kuwa kundi kubwa la mashabiki wa United hawaamini kama wanaweza kutwaa ubingwa lakini ukweli ni kwamba timu hiyo inaweza kufanya hivyo kwa kuwa sasa ipo kileleni.

 

“Huu ni ushindi mkubwa kabla timu hiyo haijavaana na Liverpool Jumapili ijayo kwenye mchezo mwingine mkubwa wa ligi hii.“Naona kuwa ni kitu kikubwa kwa kuwa ndani ya wiki sita nyuma usigeweza kufikiri kuwa United inaweza kufika hapa ilipo kwa sasa.

 

Lakini kwa jinsi walivyo na morali unaweza kuona jinsi ambavyo walikuwa wakishangilia wenyewe.“Nafikiri mashabiki wa United sasa wanatakiwa kujua kuwa wanawania ubingwa na lazima wafikiri kuhusu hilo, sijui kwa nini hawaamini lakini naona morali ya timu ipo juu sana,” alisema Neville

The post Sasa United Inawania Ubingwa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand