-->

Type something and hit enter

On
Juzi Jumanne, Januari 5, rapper #CardiB alipost picha kwenye ukurasa wake wa Instagram, lakini iliishia kupokelewa kwa maoni tofauti tofauti kutoka kwa baadhi ya mashabiki.


Wengine walidhani picha iliyo na mkono wa #Offset ikimshika rapa #CardiB sehemu ya tumbo ilikuwa kweli ni ujauzito, picha hiyo ilimlazimu #CardiB kuuzima moto mwingine wa maoni ya mashabiki kwa kuondoa dhana potofu ambayo baadhi ya mashabiki walikuwa nayo awali kuihusu picha hiyo.


Haikuishia Instagram pekee, mchanganyiko wa hofu ya ujauzito ulimwagika pia #Twitter ambapo mazungumzo hayo yaliendelea na mashabiki pia walidanganywa kuamini picha ya #CardiB ilikuwa ikiwajulisha kuwa alikuwa na mtoto mwingine njiani, lakini sivyo ilivyo.


Maapema Jana, rapper huyo mwenye umri wa miaka 28, alikomesha uvumi huo kupitia tweet yake na akiwahakikishia mashabiki wake kuwa kila mtu aliyekuwa kwenye ukurasa huo ni kwamba, #Kulture hatapata ndugu (mdogo wake) kipindi cha hivi karibuni.
Click to comment
 
Blog Meets Brand