-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison amefichua kuwa kiwango alichokionyesha katika mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan ni mwanzo kwa kuwa amejipanga kufanya mazuri zaidi bila ya kujali wanaosema vibaya.

 

Morrison amejiunga na Simba akitokea Yanga kwa mkataba wa miaka miwili lakini amekuwa akikosa nafasi kubwa ya kucheza kama ilivyokuwa Yanga kabla ya Jumatano ya wiki hii kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa Simba Super Cup.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Morrison alisema kuwa kwa upande wake hawezi kuzuia watu kusema lakini anachokiangalia kazi yake anaifanya katika ukubwa gani kwa kuhakikisha timu yake inapata matokeo ya ushindi katika kila mchezo.

 

“Kikubwa ni kuweka nidhamu na kazi, haijalishi nini kipo mbele au wangapi wanakuongelea kwa sababu nipo hapa kwa ajili ya kazi hayo mengine siyo wakati wake kwa sababu katika soka kuna mambo mengi.“

 

Lakini kikubwa ninachokiangalia kwa sasa ni kuhakikisha nakuwa bora zaidi ya mchezo uliopita, nahitaji kuwa bora zaidi ya sasa ili kusaidia timu yangu kufikia malengo yake,” alisema Morrison.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam | Championi

The post Morrison Aahidi Makubwa Simba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand