Mkude Afunika Kwa Mshahara Mnono Wazawa Bongo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Mkude Afunika Kwa Mshahara Mnono Wazawa Bongo-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

HAKAMATIKI! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mzawa anayelipwa mshahara mkubwa Bongo.

 

Wakati yeye akiongoza kwa wachezaji wazawa, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone raia wa Msumbiji ndiye anayeongoza kukunja mshahara mkubwa kwa wachezaji wazawa ambaye yeye anachukua dola 7,000 (zaidi ya Sh 16m) kwa kila mwezi.

 

Inadaiwa kuwa Mkude anakunja Sh 8m kila mwezi tangu alipoongezwa mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu wa 2018/19.

Mkude alipewa mkataba huyo baada ya kuwepo tetesi za nyota huyo kuwaniwa na Yanga katika msimu wa 2018 ambapo mkataba wake ulikuwa umemalizika kuendelea kubaki Simba.

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi fupi na ndefu juzi alisimamishwa kazi kwa kile kilichotajwa utovu wa nidhamu huku sababu ya kusimamishwa ikifi chwa.

 

Championi Ijumaa linakuletea ‘Top Five’ ya wachezaji wazawa wanaolipwa mishahara mikubwa katika Ligi Kuu Bara baada ya Mkude kuongoza ambao ni;FARID MUSSA.

 

Kiungo mshambuliaji wa Yanga ndiye anayefuatia kwa kuwa inadaiwa anakunja Sh 7m kwa mwezi tangu alipojiunga na timu hiyo katika msimu huu akitokea Tenerife FC ya Hispania.

 

JOHN BOCCO

Nahodha na mshambuliaji wa Simba anashika nafasi ya tatu kwa kulipwa Sh 7m na analipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kuongeza mkataba katika msimu wa 2018.

 

Bocco alipewa mkataba huo baada ya kuelezwa kuwa Azam FC walikuwa na mipango ya kumrejesha klabuni hapo.

ERSATO NYONI

Beki na kiungo wa Simba ambaye inadaiwa kuwa analipwa Sh 7m kila mwezi, dili ambalo alisaini mwaka 2018.

 

AISHI MANULA

Kipa namba moja wa Simba naye analipwa Sh 7m kila mwezi, naye dili lake la mwisho la mkataba alisaini mwaka 2018.Manula anapewa changamoto uwanjani na Beno Kakolanya lakini bado Manula ameendelea kuwa chaguo la kwanza kikosini hapo.

WAANDISHI: WILBERT MOLANDI, MUSA MATEJA NA MARCO MZUMBE

The post Mkude Afunika Kwa Mshahara Mnono Wazawa Bongo appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.