Michael Sarpong Atimkia China-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Michael Sarpong Atimkia China-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong ameondoka nchini kimyakimya kwenda kushughulikia matatizo ya familia yake nchini baada ya wachezaji wa timu hiyo kupewa likizo ya wiki moja ikiwa ni siku chache walipotwaa Kombe la Mapinduzi.

 

Mshambuliaji huyo ameondoka juzi usiku kuelekea kwao Ghana baada ya Yanga kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Simba kwa penalti 4-3 katika mchezo wa fainali uliopigwa Jumatano iliyopita visiwani Zanzibar.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi limezipata kuwa, mshambuliaji huyo ameondoka nchini kwenda kushughulikia matatizo ya familia yake pamoja na mambo yake mengine kabla ya kurejea tena nchini kuendelea na maandalizi ya ligi kuu na michuano mingine.

 

“Sarpong hayupo ameondoka juzi usiku kuelekea kwao kushughulikia mambo ya kifamilia kwa sababu ukiangalia ni muda mrefu hakuweza kwenda tangu kuanza kwa ligi.”

 

Yeye aliondoka baada ya ushindi dhidi ya Simba ndiyo maana hayupo katika wachezaji ambao wamerejea kutokea Zanzibar na siyo yeye hata Ninja, Makapu na Adeyum wote wamebakia Zanzibar.

 

Championi Jumamosi lilimtafuta Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze azungumzie ishu hiyo ambapo alikiri kwa kusema: “Ni kweli Sarpong hayupo aliondoka juzi kwenda kwao kwa ajili ya kuweka sawa mambo ya familia yake kwa sababu nimetoa likizo ya wiki moja kwa wachezaji kupumzika kabla ya kurejea kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya kuendelea na ligi.

The post Michael Sarpong Atimkia China appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment