-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIPA wa Simba, Aishi Manula amefunguka kuwa kikosi chao kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, FC Platinum ya Zimbabwe na kufuzu hatua ya makundi.

 

Simba inatarajiwa kuwakaribisha Wazimbabwe hao katika mchezo mkali wa marudiano unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliopigwa Zimbabwe kwa bao 1-0.

 

Simba inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ambayo hawakufanikiwa kufuzu msimu uliopita baada ya kuondolewa na UD Songo ya Msumbiji katika hatua za awali.Akizungumza na Championi Ijumaa, Manula alisema tofauti ya bao 1-0 waliyonayo mpaka sasa haiwezi kuwa kikwazo kwao kufuzu.“

 

Kwanza niseme kila mmoja anajua kuwa tuko nyuma kwa bao 1-0 mpaka sasa, lakini ni wazi bado tuna nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya makundi kwa kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa marudiano ambao tutacheza kwenye uwanja wa nyumbani hapa Dar es Salaam.“

 

Naamini matokeo mazuri kwenye michezo yetu miwili iliyopita yametuongezea morali ya kushinda mchezo huo, na kupitia sapoti ya mashabiki wetu na wadau wa soka hapa nchini tutafuzu na kwenda hatua ya makundi,” alisema Manula.

Stori: Joel Thomas,Dar es Salaam

The post Manula: Tunakwenda Makundi Afrika appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand