-->

Type something and hit enter

On 


SEXLADY kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Lulu Abasi ’Lulu Diva’ amesema hakuna kitu ambacho anakichukia kama kuweka mambo yake hadharani.

Akizungumza jana jijini Dar, Lulu Diva ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya Hauna Maajabu amesema kuwa ameshukuru sana Mungu kwa kitu ambacho amemjalia ni kuficha mambo yake, imemfanya mpaka leo watu hawajui mengi kuhusu yeye.

“Najisifu sana mimi ni mtu ambaye najua kuweka vitu kwenye siri, yaani kwa mfano ningekuwa kila kitu changu ninachoweza kukifanya natangaza mitandaoni ningekuwa super staa yani kila kona ningekuwa natajwa mimi, ila kutunza siri zako ni kitu cha muhimu sana,” alisema Lulu Diva.
Click to comment
 
Blog Meets Brand