-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa hakuna wa kumlaumu kwa kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu England mbele ya Southampton kwa kufungwa bao 1-0.

Wakiwa Uwanja wa St Mary’s walikubali kuyeyusha pointi tatu baada ya kufungwa bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa Danny Ings.Kichapo hicho kinawafanya mabingwa hao watetezi kuwa sawa kwa pointi na Manchester United ambao nao wana pointi 33 ila United imecheza mechi 16 na Liverpool imecheza jumla ya mechi 17.

Southampton wababe wa Liverpool wapo nafasi ya sita na pointi zao ni 29 baada ya kucheza jumla ya mechi 17.

Kwenye mchezo huo wa usiku wa kuamkia leo Liverpool ilipiga jumla ya mashuti 17 huku wapinzani wao Southampton wakipiga jumla ya mashuti 7 katika hayo ni shuti moja la Liverpool lililenga lango huku Southampton mashuti matatu yalilenga lango.

The post Liverpool Yapoteza EPL, Klopp Asisitiza Hana Wa Kumlaumu -Video appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand