-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MARA baada ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi cha Simba, kocha mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes, juzi usiku alifanya kikao kizito na mastaa wake wote kambini wakiwemo Junior Lokosa na Perfect Chikwende.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ko-cha huyo aanze kazi ya kui-fundisha timu hiyo ambayo jana alianza kuisimamia katika michuano ya Simba Super Cup dhidi ya Al Hilal ya Sudan.Kocha huyo amechukua mikoba ya Mbegiji, Sven Vandenbroeck aliyetimkia FAR Rabat ya nchini Morocco.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema kuwa mara baada ya wachezaji wote kuripoti kambini, aliitisha kikao cha dharura kilichohudhuriwa na benchi lote la ufundi na wachezaji ambapo kikubwa ni kuweka mikakati ya mafanikio ya kubeba mataji.

Gomes alisema kuwa kikubwa katika kikao hicho aliwataka wachezaji kutodharua mchezo wowote na badala yake wanatakiwa kushinda katika kila mchezo watakaocheza ili kufanikisha malengo yake ambayo ni kukaa kileleni katika msimamo wa ligi na kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Nimekuwa na utaratibu wa kufanya kikao na wachezaji pamoja na benchi la ufundi na kikubwa ni kuweka mikakati ya timu kufanya vizuri katika mashindano tutakayoshiriki.

 

“Kikubwa nimewaambia wachezaji wangu ni lazima tushinde katika mechi tutakayocheza ili tufikie malengo niliyoyaweka ya kukaa kileleni katika msimamo wa ligi na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kimataifa.“Ninafahamu siyo kazi nyepesi, lakini ninaamini tutafanikiwa kutokana na ubora wa kikosi nilichokikuta kilichojaa wachezaji wengi wenye ubora,” alisema Gomes anayeongea Lugha ya Kingereza na Kifaransa.

STORI: WILBERT MOLANDI | GPL

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

The post Kocha Simba Afanya Kikao Kizito na Chikwende appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand