-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema kuwa ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake kitatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi licha ya ushindani mkubwa ambao umekuwa ukionekana kwenye michuano hiyo.

 

Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itakayopigwa leo baada ya kujikusanyia pointi nne kwenye michezo yake miwili ya Kundi A ambapo ilishinda dhidi ya Namungo na kutoa sare dhidi ya Jamhuri.

Akizungumza na Championi Jumatatu,Kaze alisema: “Tumefika hatua ya nusu fainali, nawapongeza vijana wangu kwa kupambana kwa kuwa ni wazi kumekuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa timu shiriki.“Tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wa nusu fainali ili kukata tiketi ya kucheza hatua ya fainali.“

 

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa wa michuano hii ili kuzidisha morali ya kufanya vizuri zaidi pale tutakaporejea kwenye mzunguko wa pili wa ligi.”

The post Kaze: Yanga Itabeba Kombe la Mapinduzi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand