-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amesema ikiwa wataendelea kupata matokeo mazuri katika kila mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu basi hakuna atakayeweza kuzuia ubingwa ndani ya kikosi hicho kutokana na ubora waliokuwa nao.

 

Yanga chini ya Kaze imeweka rekodi mpya ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ikiwa nafasi ya kwanza na kutopoteza mchezo hata mmoja, wakishinda mechi 13, wakitoka sare mechi nne huku wakiwa na pointi 43 kabla ya mchezo wa jana Alhamisi dhidi ya Prisons.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaze alisema ana matumaini makubwa ya kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu ikiwa wachezaji wake wataendelea kujituma kwa kupata matokeo mazuri katika mechi za mzunguko wa pili baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.

 

“Kitu kikubwa kwetu ni jinsi gani tunaweza kuende-lea hapa tulipoishia katika mzunguko wa kwanza, najua ligi imekuwa ngumu na ushindani un-aongezeka kadiri unavyokutana na timu nyingine ambayo nayo imekuwa ikihitaji kupata ma-tokeo mazuri dhidi yetu.

 

“Tunataka ubingwa wa msimu huu kwa kuwa ni jambo ambalo linawezekana ingawa mzunguko wa pili unakuwa mgumu zaidi lakini hatuwezi kuacha malengo yetu ya ubingwa kwa kuwa ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu,” alisema Kaze.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaa

The post Kaze Auona Ubingwa Yanga SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand