-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Cedric Kaze raia wa Burundi, jana kililazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya kikosi cha Jamhuri kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi.Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar ulikuwa na ushindani kwa timu zote mbili kupambana kupata ushindi ndani ya dakika 90.

 

Dakika 45 za mwanzo Yanga walitengeneza nafasi zao kupitia kwa mshambuliaji Wazir Junior ambaye alikosa nafasi nne katika hizo mbili zilikwenda nje ya lango na mbili zililenga lango.

Beki Paul Godfrey, yeye alipiga shuti moja ambalo lililenga lango ila liliokolewa na kipa wa Jamhuri, Nasoro Twaliba na kufanya dakika 45 kukamilika bila kufungana ambapo Jamhuri wao walifanya jaribio kupitia kwa Ally Juma aliyepiga mashuti mawili yaliyookolewa na kipa Faroukh Shikalo.

 

Kipindi cha pili Yanga walikosa nafasi mbili za wazi za kufunga kupitia kwa Tonombe Mukoko na Michael Sarpong huku shuti la chipukizi Abubakari Yunus likiokolewa na kipa wa Jamhuri.

Mchezo wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Amaan mapema jana, Mtibwa Sugar ilishinda bao 1-0 dhidi ya Chipukizi bao pekee la ushindi kwa Mabingwa hao watetezi lilifungwa na Ibrahim Hilika.

 

Kombe la ShirikishoKatika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Namungo dhidi ya Al Hilal ya Sudan, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3 Namungo wakiwa ugenini na hivyo Namungo kufuzu kwa hatua inayofuata baada ya ushindi wa mabao 2-0 hapa nyumbani

The post Jamhuri Yaizuia Yanga Zenji, Mapinduzi Cup appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand