-->

Type something and hit enter

By On



Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa 2020 ni Haruna Niyonzima ambaye ni kiungo mshambuliaji.

 

Mechi tatu ambazo Yanga imecheza kwenye Kombe la Mapinduzi imetupia jumla ya mabao mawili kambani na imefungwa bao moja. Kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri dakika 90 zilikamilikwa kwa ubao kusoma 0-0 Uwanja wa Jamhuri.

 

Kwenye mchezo dhidi ya Namungo,Yanga ilishinda bao 1-0, mtupiaji alikuwa Zawad Mauya mtengeneza pasi Niyonzima. Kwenye mchezo huu mchezaji bora alichaguliwa kuwa Kibwana Shomari beki wa Yanga.

 

Nusu fainali ya kwanza, dakika 90 zilikamilikwa kwa ubao kusoma Yanga 1-1 Azam FC, mtupiaji kwa Yanga alikuwa Tuisila Kisinda mtengeneza pasi alikuwa ni Niyonzima.Kwenye mchezo huo Noyonzima aliibuka kuwa mchezaji bora.

 

Yanga ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 hivyo kesho inakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali itakayochezwa Uwanja wa Amaan. Niyonzima amesema kuwa furaha kubwa ni kuona timu inashinda na kufanya vizuri.

The post Huu Hapa Mtambo wa Mabao Ndani ya Yanga appeared first on Global Publishers.



Click to comment
 
Blog Meets Brand