-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

NAHODHA wa Global FC, Wilbert Molandi, amesema kuwa utapigwa mpira mwingi watakapokutana na wapinzani wao DStv katika mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Januari 30, mwaka huu.

 

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa kikosi cha Global FC, utachezwa kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Molandi ameweka wazi kwamba hakuna kitakachowazuia Global FC kusepa na ushindi kwenye mchezo huo.“Ipo wazi kabisa ushindi ni wetu kwa kuwa hakuna kitakachotuzuia tushindwe kupata matokeo mazuri, utapigwa mpira mwingi mpaka wapinzani wetu wataomba poo,” alisema.

 

Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, alisema wamejipanga kupata ushindi.“Tupo imara, unajua kwamba DStv huduma zake ni bora, hivyo hata ukitupeleka uwanjani lazima tutafanya kilicho bora, hakuna namna lazima tushinde,” alisema.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

The post Global FC na DStv Utapigwa Mpira Mkubwa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand