-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

FISTON Abdoul Razak nyota mpya wa Klabu ya Yanga amesema kuwa Yanga hawatakuwa na haki ya kumzuia kuondoka ikiwa atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili la miezi sita.

 

Nyota huyo raia wa Burundi amesaini dili la miezi sita katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15,2021 kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

 

Anaungana na nyota mwingine, Saido Ntibanzokiza ambaye naye pia ni raia wa Burundi ambaye huyu anatajwa kusaini dili la miaka miwili.

 

Habari zinaeleza kuwa Fiston ambaye ni mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza pia nafasi ya winga anasubiri dili lake jingine litiki nchini Kuwait.

 

“Miezi sita kwangu ni sawa itanipa fursa ya mimi kuondoka bila kuzuiwa pale ambapo nitahitaji, hivyo ninaamini nikifanya vizuri itakuwa njia rahisi kwangu ya kuondoka, kwenda Simba kama watanitaka, “alisema.

The post Fiston: Yanga Hawawezi Kunizuia Kuondoka appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand