-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

DILI la Doxa Gikanji wa DC Motema Pembe ya nchini DR Congo kujiunga na Simba, limeyeyuka rasmi kutokana kiungo huyo kuhitaji kushiriki michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon.

 

Gikanji ambaye anaiwakilisha Timu ya Taifa ya DR Congo, alisaini mkataba wa awali kuitumikia Simba kabla hawajaenda Cameroon kushiriki CHAN. Kitendo cha DR Congo kufuzu robo fainali ya michuano hiyo, imefanya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) yake ichelewe kufi ka Simba.

Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Simba kililiambia Spoti Xtra kuwa, kama Simba watapata ITC yake ili kukamilisha usajili wa Gikanji, basi kiungo huyo atakuwa kapoteza sifa za kuwa sehemu ya kikosi cha DR Congo ambacho jana kilicheza dhidi ya Cameroon.

 

“Doxa alikubali kusaini mkataba wa awali na Simba, lakini aliwapa masharti kuwa lazima aende kushiriki CHAN, Simba walikubali hilo lakini changamoto iliyojitokeza ni kwamba usajili ule wa CAF unakaribia kufungwa.

 

“Hivyo Simba wanatakiwa wapate ITC ya mchezaji huyo jambo ambalo kama watapewa mapema watampotezea mchezaji huyo vigezo vya kuendelea kushiriki CHAN jambo ambalo mchezaji mwenyewe hataki kuona linatokea.

 

”Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alithibitisha kuvunjika kwa dili la kiungo huyo akisema: “Usajili wa Doxa Gikanji umeshindikana maana hatuwezi kupata ITC mpaka amalize CHAN na dirisha la usajili wa CAF linakaribia kufungwa.

 

”Spoti Xtra lilimtafuta Gikanji, alisema: “Usajili wa kwenda Simba kwa sasa ni kama umekwama kutokana na mimi kuwa huku kwenye CHAN, haya yalikuwa ni malengo yangu ya kwanza kuliwakilisha taifa langu ndio maana nilisaini mkataba wa awali ili nikimaliza CHAN nimalizane nao kabisa, lakini imeshindikana kwa kuwa timu imesonga mbele na usajili wa CAF unakaribia kufungwa.“Kikubwa ni subira, bado tunawasiliana na uongozi wa Simba, huwezi jua katika usajili unaofuata tunaweza tukakubaliana tena.”

The post Dili la Gikanji Simba Layeyuka appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand