Aggrey Aagwa Kwa Heshima, Stars Yaibana DR Congo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Aggrey Aagwa Kwa Heshima, Stars Yaibana DR Congo-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Rais wa TFF Wallace Karia akimkabidhi Aggrey Morris jezi iliyosainiwa na Wachezaji, benchi la Ufundi na viongozi ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars”

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachonolewa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije jana kimelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

 

Stars ilianza kufungwa dakika ya 19 kupitia kwa Fiston Mayele bao lililodumu mpaka dakika ya 45, baada ya mabeki wa Stars kufanya uzembe kuokoa hatari na kipa mkongwe Juma Kaseja kuteleza kabla ya kuokoa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bushungwa akimkabidhi Aggrey Morris hundi ikiwa ni sehemu ya zawadi ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars”

Pongezi kwa Ditram Nchimbi ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi akichukua nafasi ya Adam Adam ambaye aliweza kubadili mchezo kwa kuongeza kasi ya ushambuliaji.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akimkabidhi Aggrey Morris Mpira uliosainiwa na Wachezaji ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya beki huyo kustaafu kuchezea timu ya Taifa “Taifa Stars”

Alitoa pasi dakika ya 56, iliyokutana na kichwa cha Ayoub Lyanga aliyeifungia Stars bao hilo murua.

 

Pia Yassin Mustapha naye alikwenda benchi nafasi yake ikichukuliwa na Edward Manyama, ambaye hakuwa na utulivu mwanzoni lakini baadaye akatulia na kuonyesha kiwango kizuri.

 

 

Kaseja naye hakumaliza dakika 90, nafasi yake ikichukuliwa na Aishi Manula, Deus Kaseke alimpisha Yusuph Mhilu. Kipindi cha pili, kiasi chake Stars ilichangamka na kufanya majaribio yaliyolenga lango tofauti na kipindi cha kwanza ambapo hawakupiga kona, shuti lililolenga lango wala lile lisilolenga lango.

Mchezo wa jana ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumuaga mkongwe Aggrey Moris ambaye alitumia dakika 3 na nafasi yake ikichukuliwa na Karlos Potrels.Mbali na kucheza mchezo huo wa mwisho nyota huyo, alipewa milioni tano kwa ajili ya pongezi kwa huduma yake Stras na jezi iliyosainiwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

 

Stars sasa inajiandaa na safari yake ya kwenda Cameroon kwenye michuano ya Chan inayoanza baadaye mwezi huu.

Stori: MARCO MZUMBEDar es Salaam

KOCHA IBENGE Afunguka KUJIUNGA na SIMBA, Aitaja YANGA, AZAM – “Ni HESHIMA KUBWA”

The post Aggrey Aagwa Kwa Heshima, Stars Yaibana DR Congo appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz