-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa utaendelea kupambana kulinda rekodi zake ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kucheza mchezo wao wa 17, leo Desemba 23, bila kupoteza.

 

Leo Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 40 inakutana na Ihefu FC iliyo nafasi ya 16 na pointi zake 13.Safu ya ushambuliaji ya Ihefu imefunga jumla ya mabao saba, inakutana na ile ya Yanga ambayo imefunga jumla ya mabao 25 ndani ya ligi.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa benchi la ufundi chini ya Cedric Kaze lipo tayari kuendeleza rekodi ndani ya ligi.“

 

Mwalimu amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu, hasa ukizingatia kwamba timu ambayo tunakutana nayo inapambana kuingia ndani ya 10 bora. Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri malengo ni kuona kwamba rekodi inaendelea kulindwa na hakika tutailinda,” alisema.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

The post Yanga Tunamaliza Mzunguko na Rekodi Leo appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand