Wanawake Kuamini Wanaume Kuwahi Kufariki - EDUSPORTSTZ

Latest

Wanawake Kuamini Wanaume Kuwahi Kufariki

 


Kumekuwa na senario ambayo imekuwa ikiendelea kwenye baadhi ya mitazamo ya watu kwamba wanaume wengi ndiyo huanza kufariki kwenye ndoa na kuacha wake zao.

 

PlanetBongo ya East Africa Radio imepiga stori na mke wa msanii Beka Flavour Happiee Reuter ambaye amefunguka kuhusiana na hilo ambapo hata yeye aliwahi kumuuliza mumewe kuwa endapo akitangulia ataiachaje familia yake.


"Wanawake tunapenda kuuliza hilo swali kwamba mume akifariki itakuaje kwa sababu tunapenda kufikiria future zaidi, wao wanafikiria leo tu kwa hiyo lazima ujiongeze, niliwahi kumuuliza  mara moja nikaona majibu yake siyaelewi"


Aidha Happiee Reuter ameongeza kusema "Kwa mfano ikitokea leo hii kadondoka ya kwetu yatakuwa nini, ndiyo maana hata mimi napambana ikitokea hayupo nisiteseke nipambane na hali yangu naogopa sana baadaye, hata yeye anaweza akafikiria ikitokea ametangulia anatuachaje, au kama ataacha magari na nyumba zigombaniwe sawa"No comments:

Post a Comment