-->

Type something and hit enter

OnKWA kinachoendelea kwa rapa, produyza na mfanyabiashara mkubwa kutoka Marekani, Swizz Beatz ni wazi kuwa
tayari ameshachizika na mikwaju ya singeli kutoka Bongo mara baada ya kuonekana mara kadhaa akiruka na mkwaju wa Chura Superstar kutoka, Meja Kunta.

 

Swizz ambaye ni mume halali wa msanii Alicia Keys, alianza kugonga vichwa vingi vya habari baada ya kuonekana akiruka na mkwaju wa Wanga ambao uliimbwa na Meja akishirikiana na Lavalava, hadi kufikia hatua watu kuamini kuwa muziki wa singeli sasa unapenya kimataifa.

 

Baada ya siku mbili tangu Chura Superstar itoke, Swizz alionekana yeye na mkewe Alicia wakicheza na kuiga kile kinachoimbwa kwenye wimbo huo, sasa hiyo tisa na kumi ni ile video inayomuonyesha mkali huyo akiwa kwenye boti huku akicheza wimbo huo kwa staili ile ile wanayocheza masela wa Temeke na Manzese.

 

Kitendo hicho cha Swizz kuonekana akisapoti mkwaju huo, kilimgusa Godfather wa Bongo Fleva, P-Funk Majani ambaye aliweka komenti kwenye moja ya posti ya Swizz na kumshukuru kwa kusapoti muziki wa Tanzania huku akimuomba kuja Bongo siku moja kwa ajili ya kuongeza kitu kwenye Bongo Fleva.Click to comment
 
Blog Meets Brand