-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BADO pointi tano tu Simba kuifi kia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara. Hiyo ni baada ya jana Meddie Kagere, mshambuliaji wa Simba, kuibuka shujaa wa kikosi hicho baada ya kufunga bao pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 75 wakati Simba ikishinda 1-0 dhidi ya KMC.

 

Kagere ambaye alianzia benchi katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, alifunga bao hilo baada ya Paul Peter wa KMC kuushika mpira katika harakati za kuokoa hatari.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, kipindi cha kwanza kilimalizika kikiwa na kosakosa nyingi lakini hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Mabadiliko ya Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck mapema tu kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili akiwatoa Aishi Manula na John Bocco huku nafasi zao zikichukuliwa na Beno Kakolanya na Kagere, yalileta ahueni na kupatikana kwa ushindi huo.

 

Ushindi huo unaifanya Simba kufi kisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, ikiwa nyuma mchezo mmoja dhidi ya vinara, Yanga pia ikizidiwa pointi tano.

Yanga ina pointi 37 ikikaa kileleni huku ikicheza mechi 15.Pia Kagere jana alifunga bao zikiwa zimepita takribani siku 72 tangu mara ya mwisho kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara.Kabla ya jana, Kagere mara ya mwisho alifunga Oktoba 4, mwaka huu, wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

 

Kagere alifunga mawili. Kwa sasa ana mabao matano, matatu nyuma ya kinara Bocco mwenye nane.

The post Simba Yafikisha Pointi 32, Yaipiga KMC Kwa Mkapa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand