-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Sadiki Momba (bukta nyeusi ) na Baina Mazola bukta (nyekundu) wakitifuana.

Bondia Baina Mazola na Sadiki Momba usiku wa kuamkia leo walitoana kijasho ulingoni kwenye mpambano wa raundi nane usiokuwa wa ubingwa uliopigwa Uwanja wa Kinesi uliopo Ubungo Shekilango Dar.

Katika pambano hilo mabondia hao walichapana vyakutosha kila mmoja akitumia maelekezo ya mwalimu wake lakini mwisho wa yote mwamuzi wa pambano hilo alitangaza matokeo ya sare.

Kama ulivyo kawaida yake mchezo wa ngumi matokeo hayo yalizua zogo kila mmoja akimtaja bondia anayemshabikia kuwa ndiye mshindi.

Mabondia hao walipohojiwa na wanahabari kila mmoja alijitapa kushinda pambano hilo na kuzidi kumtambia mwenzake hivyo kutengeneza mazingira ya kurudiwa siku nyingine.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Angalia picha

The post Sadiki Momba na Baina Mazola Walivyotoana Kijasho Ulingoni appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand