-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, anaamini kuwa Barcelona itafanya kitu kuona msimu ujao Lionel
Messi anacheza tena na Neymar ndani ya Camp Nou. Hii ni baada ya hivi karibuni, Neymar kutamka wazi kuwa msimu ujao anataka kucheza tena na Messi ingawa haijaelezwa wapi kama ni PSG au Barcelona.

 

Neymar aliondoka Barcelona mwaka 2017 na kutua PSG. Alicheza na Messi ndani ya Barcelona kuanzia 2013, tangu msimu uliopita, staa huyo amekuwa akihusishwa kurejea viunga vya Camp Nou, huku Messi mkataba wake
ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

 

“Kila mmoja anafahamu suala la Messi, mtu pekee ambaye anayeweza kuamua hatma yake kwa sasa ni yeye
mwenyewe “Klabu inapambana kuona inakuwa na wachezaji bora , nataka kuona Messi anacheza hapa na mchezaji bora (Neymar) ndani ya Camp Nou itakuwa vizuri zaidi,” alisema
Koeman.

The post Ronald Koeman Ataka Neymar Amfuate Messi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand