-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MCHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf anayekipiga katika Klabu ya Wrexham Association FC ya Wales kwa mkopo akitokea Boreham Wood FC ya England, amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi
Novemba.

 

Adi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuweka kambani mabao manne katika michezo nane aliyocheza hadi sasa, kwenye mashindano ya National League ambayo ni sawa na Ligi Daraja la Tano katika mfumo wa soka la Kiingereza ambayo ilianzishwa mwaka 1864.

 

Adi aliwahi kuitwa mara kadhaa kwenye kikosi cha Taifa Stars wakati wa kocha Emmanuel Amunike, akiwa miongoni mwa wachezaji ambao walikwenda Misri kushiriki Afcon, mwaka jana na kupata nafasi ya kucheza mechi moja.

Stori na ISSA LIPONDA

The post Nyota Taifa Stars Atwaa Tuzo Ulaya appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand