-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MAMBO ni moto kuelekea uchaguzi mdogo wa Klabu ya Simba kufuatia wanachama kujitokeza kuwania nafasi ya mwenyekiti ndani ya klabu hiyo ili kuziba nafasi ya Swedi Mkwabi aliyejiuzulu Septemba, mwaka jana.

Simba ipo mbioni kuziba nafasi ya mwenyekiti inayokaimiwa na Mwina Kaduguda ambapo uchaguzi unafatarajiwa kufanyika Februari 7, mwakani.

 

Wanachama waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni mwanahabari mkongwe na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nchemba, Juma Nkamia, Hassan Dalali, Ayubu Semvua, Victor Antony, Mohamed Soloka, Kassim Nyangalika, Rashid Shangazi, Piton Mwakisu, Hamisi Omary na Mutaza Mangungu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike, amesema: “Tunaendelea na zoezi letu la uchukuaji fomu ambalo awali lilianza kwa kulega kutokana na wajumbe kutojitokeza.“

 

Tunaamini hadi siku ya mwisho watu wengi zaidi watajitokeza kuchukua fomu ili kutimiza matakwa ya kikatiba ndani ya Simba. Nimekuwa nikipokea simu nyingi sana kutoka kwa wajumbe mbalimbali kuhitaji kuchukua fomu.”Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kufungwa Desemba 24, mwaka huu ambapo lilianza Desemba 14.

The post Nkamia Ajitosa Uchaguzi Simba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand