-->

Type something and hit enter

On
 Mkongwe wa muziki rap nchini, ambaye kila leo anaendelea kufanya vizuri kupitia muziki wake, @mwanafa amefunguka kuwa licha ya kupata Ubunge wa Jimbo la Muheza, bado ataendelea kusikika kwenye muziki.


FA ambaye anasifa yakuwa rapa anayetunga mashairi yanayo zungumzia jamii zaidi na kugusa katika kila rika, akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, amesema Rais Joh Magufuli amemwambia aendelee kutoa nyimbo.


“Kijana wa Magufuli Baba yangu ameniambia kwamba unatakiwa uendelee kuimba. Unakumbuka kuna picha tumeenda Ikulu wakati Waziri Mkuu anaapishwa (kama amenishika bega) ndio alichokuwa ananiambia, eeh bwana uendelee kutoa nyimbo, ” amesema.


“Kwa hiyo uachi muziki, muziki unakuacha, kama una vitu vya kusema, tutaendelea kusema hapa na pale,” aliongeza @mwanafa.


Ikumbukwe wimbo wa hivi karibuni kutoka kwa @mwanafa unakwenda kwa jina la "Gwiji" ambao amewashirikisha #Nyoshi na #MauaSama ambaye awali alimshirikisha kwenye wimbo uiitwao "Sielewi"


Mashairi ya kwenye wimbo wake "Gwiji" yameelezea namna ambavyo mwanaume anapambana kuhakikisha kwamba maisha yake yanaenda sawaClick to comment
 
Blog Meets Brand