-->

Type something and hit enter

On 


Leo ni Disemba 1 siku ya maadhimisho ya Ukimwi duniani, EATV & EA Radio Digital imepiga stori na mrembo Doreen Odemba kuhusu chanzo cha kutaka kujiua kutokana na ugonjwa huo.

 

Doreen Odemba ambaye amejitangaza kuishi na virusi hivyo tangu akiwa mtoto amesema alitaka kujiua kwa sababu alipitia changamoto ngumu sana wakati akiwa na umri mdogo huku akinyooshewa vidole na watu.


"Kitendo cha mimi kutaka kujiua ni kwa sababu nilipitia changamoto ngumu sana nikiwa kwenye umri mdogo, halafu watu kuninyooshea vidole kwamba nimeathirika, kibaya zaidi watu walikuwa wanamsema vibaya mama yangu kwamba kafanya moja mbili tatu kwa hiyo vikawa vinanipa mawazo na kuniumiza" amesema Doreen Odemba 


"Nikasema ili nifute hiyo aibu acha ninywe sumu na vidonge kuvikoroga ili nife lakini kumbe haikuwa mpango wa mungu kufa, Mungu ndiyo alikuwa ameniokoa unajua kama kitu ulikuwa hujakipanga yeye atakusaidia" ameongeza 


Zaidi tazama hapa chini kwenye video.
Click to comment
 
Blog Meets Brand