-->

Type something and hit enter

On
Mike Tyson bado anajutia kifo cha 2Pac Shakur, kilichotokea miaka 24 iliyopita mjini Las Vegas Nevada, Marekani.


Rapa 2Pac aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anatoka kwenye pambano la ngumi lililomuhusisha swahiba wake wa nguvu, Mike Tyson. Akifanya mahojiano na Vlad TV, Tyson amesema anajutia hadi leo kwa sababu yeye ndiye alimsukuma sana 2Pac kuja kutazama pambano lake na usiku ule ndio ukawa wa mwisho kwenye maisha yake

-

"Najihisi mwenye hatia juu yake kwa kuja kwenye pambano langu na mimi ndiye nilimshawishi sana afike. Baada ya pambano pia tulitakiwa tutoke wote. Nilimuahidi kwenda naye kwenye ukumbi wa 662 usiku ule lakini nilikuwa na mtoto mdogo hivyo mama yake alinitaka nibaki nyumbani na kweli nikabaki." alisema Tyson.

23hClick to comment
 
Blog Meets Brand