-->

Type something and hit enter

On 


Msanii wa filamu Menina Legria ameeleza kuwa wasanii kama Chidi Benz, Mr Nice na 20 Percent ndiyo walipaswa wawe na utajiri na mafanikio ili Alikiba na Harmonize wawapigie magoti maana walikuwa wamoto sana enzi zao.


Akifunguka hilo kutoka ukurasa wake wa Twitter Menina ameandika kuwa 


"Chid Benz, Mr Nice au Twenty Percent (20%) ndiyo ilipaswa wawe na utajiri na  mafanikio kama ili wakina Kiba, Chibu, Konde waje wawapigie magoti,  lakini wapi Mungu ndiye anayepanga na humpa atakaye na akitaka kukupa hakuandikii barua,  walikuwa wamoto hawa".


Aidha amefunguka kuhusu marehemu Steven Kanumba na masuala ya Bongo Movie kwa kuandika 


"Marehemu Steven Kanumba aliondoka na Bongo Movie yake, hakuna aliyeweza na anayevaa viatu vyake, waliokuwa chawa wake badala ya kuiga kazi waliiga matumizi yake leo wanasota, Lebo ya Kanumba The Great wameiua. Mama Kanumba hajafaidi 100% matunda ya mwanae"Click to comment
 
Blog Meets Brand