-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BAADA ya Yanga kumkosa beki wa kushoto, Eric Rutanga katika dakika za mwisho za usajili uliopita, hatimaye uongozi wa Yanga umerudi tena kwa Mnyarwanda huyo kwa ajili ya kumsajili kuja kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi wa kushoto la timu hiyo.

 

Yanga katika eneo la ulinzi wa kushoto kwa sasa kuna wachezaji wawili ambao ni Yassin Mustapha na Adeyum Saleh huku Yassin Mustapha akionekana kupata nafasi ya kucheza mara nyingi kumzidi Adeyum.

 

Rutanga, raia wa Rwanda, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Polisi ya nchini humo ambapo hapo awali alikuwa akikipiga katika Klabu ya Rayon Sports kabla ya kuhamia Polisi United.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, beki huyo alisema kuwa viongozi wa Yanga wameanza kumtafuta tena hivi karibuni wakiangalia uwezekano wa yeye kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la usajili.

 

“Nikiwa Rayon Sports nilitakiwa nijunge na Yanga ambao tayari tulikuwa tumeshakubaliana kwa mambo mengi lakini mwisho wa siku mambo hayakunyooka, katika dirisha hili dogo la usajili naona Yanga wamerudi tena, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hili jambo, tutaona litakavyokuwa,” alisema beki huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Mashine Hii Inakuja Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand