-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

TIMU ya Manchester United jana imetokea nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya wenyeji, West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa London. 
West Ham walitangulia kwa bao la Tomas Soucek dakika ya 38, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Paul Pogba dakika ya 65, Mason Greenwood dakika ya 68 na Marcus Rashford dakika ya 78.
Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu wanafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 10 na kupanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya nne, wakizidiwa pointi tatu na vinara, Chelsea ambao hata hivyo wana mchezo mmoja zaidi, wakati West Ham inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya saba baada ya mechi 11
 


Click to comment
 
Blog Meets Brand