-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
MANCHESTER United ilitumia dakika mbili za mwsho kujikatia tiketi ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup kwa mabao ya Edinson Cavani dakika ya 88 na Anthony Martial dakika ya 90 na ushei ikiwalaza wenyeji, Everton 2-0 Uwanja wa Goodison Park. 
Mechi nyingine ya Robo Fainali ya Carabao Cup jana, Tottenham Hotspur iliwachapa wenyeji wengine, Stoke City 3-1 Uwanja wa bet365, Stoke-on-Trent, Staffordshire.
Ikumbukwe jana Manchester City iliichapa Arsenal 4-1 Uwanja wa Emirates, London na Brentford ikichapa Newcastle United 1-0 Uwanja wa Brentford Community.
Sasa Manchester United itacheza na Manchester City katika Nusu Fainali Januari 5, 2021 uwanja wa Old Trafford, wakati Tottenham Hotspur itamenyana na Brentford 


NUSU FAINALI: Januari 5, 2021
Saa 8:00 mchana
Manchester United   Manchester City
Saa 2:00 usiku
Tottenham Hotspur   BrentfordClick to comment
 
Blog Meets Brand