-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
MABONDIA nyota wa Tanzania jana waliwashinda wapinzani wao kutoka nchi tofauti kwa staili mbalimbali katika ukumbi wa Next Door Arena – Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ akiwa kivutio zaidi baada ya kumshinda Symon Tcheta wa Malawi kwa KO raundi ya kwanza.
Mfaume Mfaume alishinda kwa pointi dhidi ya Chikondi Makawa wa Malawi sawa Ismail Galiatano aliyemshinda Israel Kamwamba wa Malawi pia, wakati Tonny Rashid alimpiga Hassan Milanzi wa Zimbabwe kwa KO raundi ya pili, Selemani Kidunda akamchapa Limbani Masamba wa Malawi pia kwa KO raundi ya pili.
Mpinzani wa Twaha Kiduku, Guy Tshimanga Tshitundu kutoka Kongo hakutokea, wakati Juma Choki akamchaka Issa Nampepeche kwa TKO raundi ya tatu katika pambano la watoto wa nyumbani.Click to comment
 
Blog Meets Brand