-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

IMEFICHUKA kuwa rekodi ya kufunga mabao 25, ndani ya kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars ndiyo imekuwa sababu kubwa ya klabu ya soka ya Gwambina kuvutiwa na mpango wa kumsajili nyota wa zamani wa Klabu ya Yanga, Mrisho Ngasa.

 

Ngasa anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ndani ya kikosi cha Stars kwa wachezaji wa kizazi cha sasa akiwa ameweka kambani mabao 25, akizidiwa mabao matatu tu na mfungaji bora wa muda wote ndani ya kikosi hicho, Sunday Manara ambaye ana mabao 28.

Ngassa alikuwa sehemu ya wachezaji 14 walioachwa na Yanga Agosti 3, mwaka huu.Akizungumza na Championi Jumatano,Mratibu wa Mashindano wa Gwambina, Mohamed Almas alisema usajili wa nyota huyo ni mapendekezo ya Kocha Mkuu, Fulgence Novatus na Mkurugenzi wa Ufundi, Mwinyi Zahera.“

 

Suala la usajili wa Ngassa limekamilika kwa kiwango kikubwa na kama kila kitu kitawekwa sawa basi hivi karibuni atatangazwa rasmi, usajili wake ni mapendekezo ya Kocha Novatus ambao umethibitishwa na mkurugenzi wetu wa ufundi, Zahera.“

 

Kimsingi tunatarajia matokeo makubwa baada ya kukamilisha usajili huu, kwa kuwa Ngassa ni mchezaji mkubwa na hata takwimu zinambeba ambapo mpaka sasa ni mfungaji bora wa muda wote wa Stars kwa vizazi vya sasa akiwa amefunga mabao 25, lakini hata mchango wake kwenye mafanikio ya klabu nyingine ni mkubwa,” alisema.

 

Gwambina inakamatia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 16.

Stori: Joel Thomas,Dar es Salaam

The post Mabao 25 Yampeleka Ngassa Gwambina appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand