-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA wa FC Platinum ya Zimbabwe, Norman Mapeza ni kama ameingia mchecheto kuelekea katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba, kufuatia kuzuia wachezaji kutumia simu katika kipindi cha maandalizi ya mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumatano.

 

Simba ipo Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu hiyo anayochezea Mtanzania, Elias Maguli katika mchezo ambao umepangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Harare nchini humo.

 

Taarifa kutoka nchini humo zinasema kocha wa timu hiyo, amepiga marufuku matumizi ya simu kwa wachezaji wote katika kipindi chote cha maandalizi ya kuelekea katika mchezo Kisa Simba, wachezaji FC Platinum wapokwa simu mwao huo kwani wanachotaka ni kuweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

 

Simba wamefi ka mapema kuzoea mazingira lakini hiyo ni kama imemshtua kocha wa FC Platinum, kwa sababu amezuia matumizi ya simu kama wachezaji walivyokuwa wakifanya chini ya kocha ambaye alifukuzwa kabla ya kuanza michuano ya kimataifa.

“Sasa hawaruhusiwi kutumia simu wakati wanakwenda mazoezini wachezaji wote wanaacha katika vyumba vyao wala wakati wa kula, ikigundulika unatumia simu kwa kujifi cha hiyo inakuwa ni ishu nyingine kabisa, ameongeza umakini kutokana na ukubwa wa mchezo wenyewe wanaokwenda kucheza Jumatano,” alisema mtoa taarifa.

 

Championililimtafuta mshambuliaji wa timu hiyo, Mtanzania, Elias Maguli ambaye alisema: “Kwanza nadhani hatuna presha kuelekea katika mchezo huo na kuhusu hiyo ishu ya simu nadhani ni utaratibu wa kawaida ambao kocha mwenyewe amejiwekea.

IBRAHIM MUSSA,Dar es Salaam

The post Kisa Simba, Wachezaji FC Platinum Wapokwa Simu appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand