Kina Mdee wadaiwa kuandaa kongamano Bawacha, mwenyewe akanusha - EDUSPORTSTZ

Latest

Kina Mdee wadaiwa kuandaa kongamano Bawacha, mwenyewe akanusha

 Dar es Salaam. Wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa Chadema, wanadaiwa kuandaa kongamano la wanawake kinyume na maelekezo ya chama hicho ya kuwakataza kutoshiriki shughuli zozote za chama.


Wabunge hao wanaoongozwa na Halima Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha) walifukuzwa uanachama Novemba 27, baada ya kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa bila kufuata utaratibu wa chama hicho.


Kulingana na taaarifa iliyotolewa jana na makamu mwenyekiti Bawacha Zanzibar, Sharifa Suleiman, wabunge hao 19 wamewapigia simu wanawake wa baraza hilo wakiwashawishi kushiriki kwenye kongamano hilo ambalo halikuwekwa wazi litafanyika lini.


Alisema chama chake hakijaandaa kongamano hilo la wanawake, ila Mdee na wenzake wanataka kuwashawishi wanawake wa Chadema washiriki ikiwa ni kutafuta jukwaa la kuonyesha kuwa wanaungwa mkono.


“Tumepata taarifa wanatumia nembo na jina la Chadema kuwahadaa baadhi ya viongozi na kina mama wa Bawacha kwa fedha na ahadi za mitaji ya biashara na mafunzo ili wafike Dar es Salaam kwenye kongamano.


“Mwanachama yeyote atakayeshirikiana na watu hawa 19 atambue atakuwa anakiuka taratibu na maamuzi ya chama na atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya chama cha mwongozo wa Bawacha,” alisema Sharifa.


 Makamu mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mbali na kuendelea kufuatilia nyendo za Mdee na wenzake, baraza hilo limewataka wajumbe wake kuwa imara wakati wanaendelea kujipanga kutekeleza maagizo ya kamati kuu ya kuziba pengo la hao 19 waliovuliwa uanachama.


Akizungumza na gazeti hili, Mdee alikanusha kuhusu taarifa hiyo na kuwataka wanawake wa Bawacha kujikita kwenye kujenga chama na kuachana na majungu. “Mimi kwa sasa nashughulika na rufaa ya Baraza kuu, hizi habari za kuokoteza sina muda wa kuzifanyia kazi, ni habari za uzushi. Sisi tumeheshimu uamuzi wa chama, tuko kwenye muda wa rufaa.


“Kama nikitaka kufanya shughuli za kijamii sishindwi. Nawashauri viongozi wa Bawacha waliobaki walijenge baraza ambalo sisi tulipambana kujijenga mpaka limepata heshima, waachane na Mdee,” alisema Mdee.


Alisema maelekezo ya chama yalikuwa wazi kwao kwamba wasifanye shughuli za chama na yeye kwa sasa si mwenyekiti, bali ni mwananchi wa kawaida.


Kuhusu muda wa rufaa alisema: “Bado tuko ndani ya muda wa rufaa. Katiba ya Chadema inasema siku 30 baada ya kupata taarifa ya maandishi. Tulipata taarifa Novemba 30, ikifika Desemba 29 ndiyo mwisho, ndipo mtuulize.”
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.