-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amefunguka kuwa anajua kazi ya kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’, ndiyo maana alipendekeza asajiliwe huku akiwataka mashabiki wa timu huyo kutulia ili waone ubora wake.

 

Ntibazonkiza, raia wa Burundi, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa mchezaji huru, licha ya kufanya mazoezi na Vital’O ya Burundi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema kuwa yeye ndiye aliyependekeza usajili wa mchezaji huyo kwa kuwa anajua ubora wake lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo watulie ili waone ubora wake baada ya kuanza mazoezi na timu hiyo.

 

“Ni mchezaji mzuri, najua kwa nini nilipendekeza aje hapa kwa sababu nafahamu ubora na uzoefu wake, ndiyo tunautaka ndani ya timu yetu na tayari ameanza kuonyesha kitu cha tofauti katika mazoezi ambayo tunafanya.

 

“Jambo la msingi kwa sasa ni kwa mashabiki wetu watulie na wampe muda ili waweze kuona kile ambacho anacho ndani ya mechi zetu kwa sababu tunataka kuendelea kubakia juu, nguvu yake inahitajika katika mapambano yetu msimu huu,” alisema Kaze.

 

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

 

 

The post Kaze: Naijua Kazi ya Saido, subirini Shoo! appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand