Jinsi ya Kushiriki na Shirika la EYP Katika siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia - EDUSPORTSTZ

Latest

Jinsi ya Kushiriki na Shirika la EYP Katika siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Empower Youth Prosperity (EYP)
Empower Youth Prosperity (EYP) 


Jinsi ya Kushiriki na  Shirika la  EYP Katika siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia 

Shirika la Empower Youth Prosperity (EYP) limewatangazia Umma na wadau mbalimbali wanaopinga ukatili juu ya watoto wa kike na wanawake Kushiriki kwa pamoja siku 16 za kupinga manyanyaso hayo dhidi ya watoto wa kike na wanawake Ulimwenguni. Soma zaidi pia>>>>>EYP MGUU KWA MGUU ELIMU JUU YA CORONA NCHINI

Empower Youth Prosperity (EYP) imelenga kufanya maandamano  ya amani pamoja na vijana wenye nia ya kuihamisha jamii kupata uelewa juu ya siku 16 pia  jamii ielewe mila na desturi kandamizi dhidi ya mwanamke na binti wa kike hasa katika masuala ya Elimu pamoja na afya.

Maandamano hayo yataafanyika mkoani mbeya  tarehe 09 Disemba, 2020 katika junction ya Mafyati mpaka mnarani kuanzi saa 09:00 mpaka 10:00AM

Jinsi ya Kushiriki

Njia ya kushiriki


Kushiriki  katika maandamano Haya ya Amani, jaza form iliyoambataniswa hapa chini au 

kupitia kwenye mitandao ya kijamii kwa  kupost Jumbe za kupinga ukatili huu na kuweka hastag ya #Empoeryouthprosperity #EYPZeroGBVinaanzanamimi

Bofya Hapa  kujiunga kwenye vuguvugu hili.

USICHOKIJUA KUHUSU SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Empower Youth Prosperity (EYP)
Empower Youth Prosperity (EYP

Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia ni kampeni  ya Kimataifa  inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991. Chimbuko la 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya kinyama ya kina dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960. Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 iwe siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa Desemba 10 ya kila mwaka. SOMA PIA MAAFISA WA EYP WATOA ELIMU YA KUMBANA NA CORONA MKOANI SINGIDA

Siku hizi 16 hutoa mwanga wa uelewa kwa jamii kwa siku nyingine muhimu kama Novemba 29 ambapo ni siku ya Kimataifa ya watetezi wa haki za Wanawake , Desemba 1,Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba 6 siku ya mauaji ya kikatili ya Montreal 1989 (wanawake 14 waliuawa na mtu aliyekuwa anawachukia wanawake) na Desemba 10 siku ya Haki za Binadamu Duniani.

Lengo la maadhimisho haya ni kutoa fursa kwa wanawake, wanaume,Vijana wa kike na kiume na wanaharakati wengine kukuza uelewa wa umma juu ya mchango wa wanawake katika maendeleo na kutafakari matokeo ya harakati za ukombozi wa mwanamke Kimapinduzi sambamba na kutafakari mafanikio hayo kwa miaka 20 ya tangu kuanzishwa kwa harakati hizo nchini mwaka 1993 TGNP ilipoanza.

Tutakumbuka kuwa maadhimisho haya huanza Novemba 25, ambayo ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake hadi Desemba 10 ambayo ni Siku ya Haki za Binadamu Ulimwenguni.  Siku hizi 16, TGNP na mashirika mengine yanayotetea haki, usawa wa Kijinsia na ulinzi dhidi ya makundi yaliyoko pambezoni hasa wanawake  wanaadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwepo kusikiliza visa mkasa, kutoa shuhuda hadharani, kushirikina na mamlaka za kiserikali na dola latika kuunganisha nguvu kutokomeza kabisa Uakatili wa Kijinsia

No comments:

Post a Comment