-->

Type something and hit enter

On
Rihanna na A$AP Rocky wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi, umethibitisha mtandao wa Page Six pamoja na mitandao mikubwa ya habari za burudani nchini Marekani.


Tovuti hiyo imeeleza kwamba imewanasa wawili hao wakila chakula cha usiku pamoja na marafiki mjini New York, Jumamosi wiki iliyopita.


Kabla ya uthibitisho huu, Riri na Rocky walikuwa wakihisiwa muda mrefu kuwa kwenye mahusiano, hii ni tangu Rihanna aachane na bilionea Hassan Jameel mapema mwaka huu. Ukaribu wao ulianza tangu mwaka 2013.


Hivi karibuni walishirikiana kwenye kampeni ya Fenty Skin line na walifanya mahojiano na Jarida la GQ na Vogue kwa ajili ya promosheni.

 Click to comment
 
Blog Meets Brand