-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema tatizo kubwa lililopo Kwenye timu yake kwa sasa ni ubutu wa washambuliaji wake kushindwa kufunga jambo ambalo linahitaji muda kutafutiwa dawa.

 

Usiku wa kuamkia leo Manchester City ikiwa Uwanja wa Etihad ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na West Brom na kuwafanya wagawane pointi mojamoja kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

 

Likay Gundogan alipachika bao la Kwanza kwa City dakika ya 30 na dakika ya 43 Ruben Dias alijifunga na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.

 

Guardiola amesema kuwa walimiliki mchezo katika kila kitu ila walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kipindi cha Kwanza na kipindi cha pili jambo lililowafanya washindwe kupata ushindi.

 

“Tulostahili kushinda kwa kuwa tuliweza kumiliki mchezo. Kwa namna ambavyo tumefanya nadhani tumepiga mashuti 26 ila haikuwa nzuri kwetu hivyo tunapambana kutafuta matokeo,” amesema.

 

The post Guardiola Alia na Washambuliaji Wake appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand