-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WAKATI Simba ikiondoka jana kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum utakaopigwa Jumatano ijayo, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa utafanya juu chini kwa kuhakikisha wanapata ushindi wa kutosha ili uwe faida kwao katika mchezo wa marudiano utakaopigwa hapa nchini.

 

FC Platinum anayochezea Mtanzania, Elias Maguri inatarajia kucheza na Simba katika mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo Jumatano ijayo katika mchezo ambao Simba itaanzia ugenini.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, msemaji wa timu hiyo, Chido Chizondo alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa kuhakikisha wanapata matokeo makubwa katika mchezo huo kwa kuwa wanatambua ubora wa Simba inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.“

Tumejiandaa kupata matokeo mazuri, namaanisha ushindi mkubwa ambao kwetu hauwezi kuwa kikwazo katika mchezo wa marudiano, tunajua kwamba Simba ni bora lakini tutakuwa bora kwa sababu tunaanzia kwetu.

 

“Nadhani kikubwa ni kwamba tunaelewa Simba ni timu ya aina gani kutokana na kuweza kutumia vyanzo vyetu kufahamu baadhi ya mambo muhimu lakini tunaelewa kuna baadhi ya maofisa wao wameshaingia Zimbabwe ila hatuwezi kuhofia chochote,” alisema Chizondo.

The post FC Platinum Wawawekea Mkakati Mzito Simba appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand