Dalali: Wanachama Wamenipa Milioni Nigombee Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Dalali: Wanachama Wamenipa Milioni Nigombee Simba-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, amesema kuwa, wanachama zaidi ya 50 wamemfuata kumtaka kuwania nafasi ya uenyekiti ndani ya klabu hiyo ambapo tayari ameshafanikiwa kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo.

 

Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba, imetangaza uchaguzi mdogo ndani ya klabu hiyo kwa ajili ya kuziba nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti, Swedi Mkwabi aliyeachia madaraka Septemba, mwaka jana ambapo nafasi hiyo ilikaimiwa na mjumbe wa kamati ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mwina Kaduguda.

 

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Februari 7 mwakani ambapo zoezi la uchukuaji fomu limeanza Desemba 14 na litafungwa Desemba 24 huku wajumbe watatu wakijitokeza kuchukua fomu hizo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Dalali alisema kuwa, ameamua kuchukua fomu hiyo kutokana na kukidhi vigezo na ni haki yake kisheria kutokana na kanuni ya TFF ambayo inaruhusu mgombea mwenye elimu ya kidato cha nne.

 

“Nimechukua fomu jana kutokana na wanachama kunifuata nyumbani kwangu kuhitaji nifanye hivyo ambao wamenichangia fedha ya kwenda kuchukulia fomu kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000).

 

“Haina shida iwapo mimi nilikuwa mwenyekiti awali kwa kuwa sikuongoza miaka nane mfululizo, kikanuni inaeleza kuwa iwapo umekuwa mwenyekiti kwa muda wa miaka minne kisha ukaishia hapo na ukakaa pembeni na ukihitaji kugombea tena unaruhusiwa, nisingeweza kuruhusiwa kugombea iwapo ningekuwa nimeongoza kwa miaka nane mfululizo, kipindi kile sikuweza kugombea kutokana na vigezo vilivyowekwa vya elimu ya digrii lakini sasa uchaguzi unakwenda kwa mujibu wa kanuni ya TFF ambayo inaruhusu mtu kugombea akiwa na elimu ya kidato cha nne,” alisema Dalali.

 

Aidha miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na Mohamed Soloka, Ayubu Semvua na Dalali.

KHADIJA MNGWAI, Dar es Salaam

The post Dalali: Wanachama Wamenipa Milioni Nigombee Simba appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.