CAS Yampiga Stop Morrison, Yanga Wachekelea-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

CAS Yampiga Stop Morrison, Yanga Wachekelea-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIMENUKA! Ndivyo utakavyoweza kusema baada ya Mahakama ya Usuluhishi ya Masuala ya Soka ya Kimataifa (CAS) kumtumia barua ya kumsimamisha kiungo mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison kucheza soka hadi pale kesi yake itakaposikilizwa upya na hukumu kutolewa.

 

Hiyo ni baada ya Yanga kupeleka mashitaka yao CAS ikiomba sakata hilo kusikilizwa upya baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuamuru Morrison kuichezea Simba.

 

Kamati hiyo iliamuru Mghana huyo kuichezea Simba baada ya kubaini mkataba wake wa awali na Yanga kuonekana una mapungufu, maamuzi hayo yaliwafanya viongozi wa Yanga kukimbilia CAS kwenda kukata rufaa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka ndani ya Simba, CAS imemtumia barua kiungo huyo ikimtaka kutoendelea kuitumikia timu hiyo katika mashindano yoyote ikiwemo Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mtoa taarifa huyo alisema zaidi ya wiki moja na nusu sasa zimepita tangu kiungo huyo mwenye mbwembwe za kuupandia mpira kupokea barua hiyo ya kumzuia kuichezea Simba hadi pale kesi hiyo itakaposikilizwa na hukumu kutolewa na CAS.

 

Aliongeza kuwa, hiyo ndiyo sababu ya Simba kumuacha kiungo huyo kwenye safari ya Mbeya wakati Simba ilipokwenda kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, pamoja na Zimbabwe walipokwenda kucheza dhidi ya FC Platinum katika Ligi ya Mabingwa Afrika, huku pia akiukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

 

“Ukweli wa Morrison kuachwa kwenye msafara wetu uliokwenda kucheza dhidi ya Mbeya City mkoani Mbeya pamoja na huu wa Zimbabwe ni baada ya kupokea barua kutoka CAS.“

 

CAS walimtumia shauri la kusikilizwa kesi yake upya baada ya Yanga kumkatia rufaa wakiomba kusikilizwa upya kesi hiyo ambayo imekaa vibaya baada ya mahakama hiyo kumsimamisha kuitumikia Simba hadi pale itakaposikilizwa kesi hiyo na hukumu kutolewa.“

Hiyo ndiyo sababu kubwa ya Morrison kutokuwa sehemu ya mechi zetu kwa sasa, hakuna kingine,” alisema mtoa taarifa huyo.Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, alisema: “Suala la YANGA ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2014/15 kwa kukusanya pointi 55 huku ikipoteza michezo miwili ya mwisho dhidi ya Ndanda na Azam.SIMBA kwa msimu wa 2010/11, ilishikilia rekodi ya kukusanya pointi nyingi kwenye michezo ya ugenini ambazo ni 29.

 

FATUMA Mustapha wa JKT Queens, ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Wanawake akiwa amefunga 14.

 

Mido Mnigeria aliyefuatwa na Simba huyu hapaUONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, upo katika mazungumzo na moja ya mchezaji kutoka Nigeria ambaye watamsajili kupitia kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Tayari Simba kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo imemsajili kiungo raia wa Uganda, Thadeo Lwanga.Hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alithibitisha kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya mazungumzo na mchezaji huyo.

Spoti Xtra limebaini kwamba, kiungo huyo ni Oche Ochewechi wa Plateu United ambaye mwenyewe amekiri kuwa kwenye mazungumzo na Simba.Akizungumza na Spoti Xtra, Oche Ochewechi alithibitisha kuhitajika ndani ya Simba huku akikiri kuwa kwenye mazungumzo na timu hiyo.

 

“Uongozi wa Simba umenitafuta, tumezungumza mambo mengi lakini kubwa zaidi ni kuhusu masuala ya usajili, bado hatujamalizana lakini hadi sasa tunaendelea na mazungumzo, nadhani jambo zuri ni kusubiri kuona mazungumzo yataishia wapi kwa kuwa bado hatujamalizana,” alisema mchezaji huyo.

 

Mbali na mchezaji huyo, pia Simba inahusishwa na kiungo mwingine Mnigeria anayekipiga katika Klabu ya Plateau ya nchini huko, Issa Ndala ambaye pia amekuwa akihusishwa kuhitajika ndani ya Yanga.

 

Morrison tumelifikisha CAS baada ya TFF kumuamuru mchezaji huyo kuwa mali ya Simba, sisi tumeenda huko lengo ni kupata haki ambayo ninaamini tutapata.”

 

Morrison ambaye aliitumikia Yanga kwa takribani miezi sita, msimu huu alijiunga na Simba ambapo usajili wake huo ulileta mvutano mkubwa kiasi cha kufikishana TFF ambapo shirikisho hilo lilitoa majibu ya kwamba mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote baada ya kubaini mapungufu kwenye mkataba wake na Yanga.

STORI: MARCO MZUMBE, DAR ES SALAAM

The post CAS Yampiga Stop Morrison, Yanga Wachekelea appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.