-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, alikuwa katika benchi akishuhudia timu yake ikipata kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya PSG, juzi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Pamoja na kipigo hicho, kuna jambo limeibuka kuwa katika mchezo huo kiungo wa United, Bruno Fernandes inadaiwa alikuja juu na kufoka akitaka kocha afanye mabadiliko wakati mchezo ukiendelea.

 

Picha zinamuonyesha Bruno akifoka huku akionyesha ishara ya kunyanyua mkono, japo bado uhakika wa nini alichokuwa akifoka lakini inadaiwa alikuwa akitaka atolewe mshambuliaji Marcus Rashford ambaye alikuwa
ameumia.

 

Kipigo hicho kilichotokea kwenye Uwanja wa Old Trafford, kimeiacha United katika wakati mgumu katika mbio za kufuzu hatua ya mtoano kwa kuwa timu tatu kati ya nne zinalingana
pointi.

 

Mashabiki wengi wa United mtandaoni wameonekana wakimshushia lawama Ole kuwa alikuwa mgumu kufanya
maamuzi ya mabadiliko  kuanzia kwa Fred ambaye hakuwa na mchezo mzuri mwisho akapata kadi
nyekundu.

The post Bruno Amjia Juu Ole appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand