Bosi Simba Ataja Sababu za Kuwatupa nje Plateau-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Bosi Simba Ataja Sababu za Kuwatupa nje Plateau-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MKURUGENZIMtendaji Mkuu wa Simba (C.EO), Barbara Gonzalez, ametamba kuwa wana kila sababu ya timu yao kufika hatua ya makundi ya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf) huku akitaja sababu tano za wao kufikia huko kwenye msimu huu.

 

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo kwa kuwaondoa Plateau United ya nchini Nigeria.

Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa New Jos, nchini Nigeria bao lililofungwa na Mzambia Clatous Chama, kabla ya kuja kutoa suluhu nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kuipa nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

 

Kwa mujibu wa Barbara, aliwapongeza vijana wao kwa kufuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kupambana katika michezo yote miwili licha ya nyumbani kupata suluhu huku akitaja sababu ya kwanza ni :“Tuna kikosi bora tulichokiboresha kwenye misimu mitatu na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo.“

Pili, tuna kocha na benchi la ufundi lililokuwa bora likiongozwa na Sven (Vandenbroeck) aliyeipa ubingwa wa Ligi na Kombe la FA msimu uliopita akiwa na msaidizi wake Matola (Seleman).

 

“Tatu, tuna mashabiki wana uzalendo na timu yao ambao wenyewe kila nchi na mkoa wanasafiri na timu kwa ajili ya kuwasapoti wachezaji wao wakiwa uwanjani wakiipambania timu yao.

 

“Nne, tuna uongozi na bodi yenye uweledi mkubwa wanapambana kila kona kuhakikisha timu inapata mafaniko zaidi ni matokeo ya ushindi katika kila mchezo utakaokuwa mbele yetu.“Tano, timu yetu imekamilika kila idara kwa kuanzia safu ya ulinzi kwa maana ya makipa, mabeki, viungo na washambuliaji watakaoamua matokeo katika mechi,” alisema Barbara.

STORI: WILBERT MOLANDI, CHAMPIONI JUMATANO

The post Bosi Simba Ataja Sababu za Kuwatupa nje Plateau appeared first on Global Publishers.No comments:

Post a Comment