-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez, tayari ameanza maandalizi ya msimu wa 2021/2022 na juzi alikuwa kwenye Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kutafuta vifaa vipya vya timu.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu bosi huyo atoke kufanya ziara ya kujifunza na kutembelea Makao Makuu ya Klabu ya Zamalek jijini Cairo, Misri.

 

Katika ziara hiyo iliyokuwa ya kujifunza jinsi ya uendeshaji wa klabu na kujenga mahusiano mazuri, aliongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Ng’ambi.

Kwa mujibu wa Barbara, yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu ujao na kikubwa kutafuta vifaa kama jezi, vifaa vya mazoezi na kadhalika.

 

Barbara alisema kuwa kabla ya kusafiri kwenda Sauz, alijadiliana na kocha katika kutafuta vifaa vingine tofauti na jezi watakavyovitumia mazoezini na kwenye mechi.

“Tunajiandaa na msimu wa 2021/2022 mapema.

 

Jana nimezunguka Joberg (Johannesburg) kutafatuta vifaa vipya kwa timu yetu kwa majadiliano na kocha; pia tumewasiliana na washiriki mbalimbali kuweza kupata chaguo na miundo ya jezi.

 

Ukianza mapema, utapata kila unachokitaka!” alisema Barbara.Simba kwenye msimu huu, imetoa matoleo mawili ya jezi tofauti, kati ya hizo zipo wanazozitumia kwenye Ligi Kuu Bara na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo walianza kuzitumia walipocheza dhidi ya Plateau United ya nchini Nigeria.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

The post Bosi Simba Afuata Vifaa Vipya Sauz appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand